• 6 years ago
Wimbo wa Kuabudu "Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu" | The Manifestation of the Power of God

Mungu aliumba vitu vyote, na hivyo Yeye hufanya viumbe vyote
kuja chini ya amri Yake, na kutii utawala Wake.
Anaamuru vitu vyote, akividhibiti katika mikono Yake.

Vitu hai, milima, mito na mwanadamu lazima vyote vije chini ya amri Yake.
Vitu angani na duniani lazima vyote vije chini ya utawala Wake.
Vyote lazima vitii, bila uchaguzi wowote.
Hii ni amri ya Mungu na mamlaka Yake.

Mungu aliumba vitu vyote, na hivyo Yeye hufanya viumbe vyote
kuja chini ya amri Yake, na kutii utawala Wake.
Kila kitu kinaamuriwa na Mungu. Anaamuru na kuvipanga vitu vyote,
kila kuainishwa kulingana na aina na kwa mapenzi ya Mungu kupewa nafasi yake.
Vitu angani na duniani lazima vyote vije chini ya utawala Wake.
Vyote lazima vitii, bila uchaguzi wowote. Hii ni amri ya Mungu na mamlaka Yake.

Haijalishi kitu ni kikubwa vipi, hakitaweza kamwe kumzidi Mungu.
Vyote vinamtumikia Mungu-hakuna binadamu wanaothubutu kupinga au kufanya madai kwa Mungu.
Mwanadamu, kiumbe wa Mungu, lazima pia aendeleze wajibu wake.
Awe bwana au mtawala wa vitu vyote, hata hadhi yake iwe ya juu vipi,
mtu mdogo chini ya utawala wa Mungu atabaki kuwa.
Mwanadamu asiye na maana, kiumbe wa Mungu, kamwe hatakuwa juu ya Mungu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Injili ya Kushuka kwa Ufalme: https://sw.kingdomsalvation.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu: https://sw.godfootsteps.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu YouTube: https://www.youtube.com/channel/UCkUDnudSY6_KR123N2Yr7mw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Facebook: https://www.facebook.com/kingdomsalvationsw/
Kanisa la Mwenyezi Mungu Twitter: https://twitter.com/CAGchurchsw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Instagram: https://www.instagram.com/thechurchofalmightygodsw/
Kanisa la Mwenyezi Mungu Vimeo: https://vimeo.com/thechurchofalmightygodsw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Blogger: http://nikanisalamwenyezimungu.blogspot.com/

Recommended