Magoli yote: Yanga ilivyoipa Alliance kipigo cha mabao 3-0 (TPL – 20/10/2018)

  • 6 years ago
Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Bara Yanga SC leo wameiduwaza Alliance kwa kuwa kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga licha ya kuzidiwa umiliki wa mpira, walianza kuishushia kichapo Alliance dakika ya 18 ya mchezo kupitia kwa Heritiel Makambo akimalizia kwa kichwa krosi ya Ibrahim Ajibu.

Ajibu pia alihusika kwenye bao la pili kwa kutoa pasi ya mwisho kwa Mrisho Ngasa aliyefunga bao la pili dakika ya 25.

Deus Kaseke aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa, alitoa pasi ya mwisho kwa Ibrahim Ajibu dakika ya 86, ambaye alifunga bao la tatu na kukamilisha ushindi huo mnono wa Yanga ukiwa ni ushindi wa sita kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Category

🥇
Sports

Recommended