Uchunguzi wa DNA wabaini 99% ‘Jowie’ alikuwa eneo la mauaji

  • 6 yıl önce
Mshukiwa mkuu wa mauaji  ya Monica Kimani aliyeuawa kinyama katika nyumba yake mtaa wa Kilimani Joseph Irungu almaarufu Jowie sasa amejipata pabaya baada ya chembe chembe za dna kutoka kwa mwili wa marehemu Monica kudhihirisha wazi kuwa alikuwa kwenye eneo la uhalifu.
Chembe chembe za dna kwenye nyumba ya Monica ziliambatana asilimia 99 na zile za mshukiwa jowie huku wanasiasa wawili waliozungumza na mshukiwa kupitia ujumbe mfupi wa simu, wakitarajiwa kufika kwenye idara ya upelelezi kuandikisha ripoti kama anavyoarifu sasa Angela Cheror.