Mbowe "Huu ndio uzembe uliosababisha kuzama MV Nyerere, Rais Magufuli chukua hatua"

  • 6 years ago
Leo Septemba 21, 2018 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema ajali iliyotokea Ukerewe jijini Mwanza ya kuzama Kivuko cha Mv Nyerere ni ya kizembe.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambapo amesema wanamtaka Rais John Magufuli achukue hatua kwa watendaji wake.