KIMENUKA! Magufuli Kamtolea Uvivu Paul Makonda sakata la Makontena

  • 6 years ago
Rais John Magufuli amewataka viongozi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria pamoja na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wakati akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa wilaya hiyo.

Amesisitiza kuwa viongozi wote wajenge utaratibu wa kusoma sheria na kujiepusha kutumiwa kwa maslahi ya watu binafsi. Rais Magufuli ametolea mfano mgogoro wa makontena yanayodaiwa kuwa na samani za shule na yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) katika bandari ya Dar es Salaam na kusema kuwa makontena hayo yanapaswa kulipiwa kodi kwa mujibu wa sheria.

Usipitwe na Matukio Muhimu kutoka Kenya, Tanzania na Uganda kwa Lugha ya Kiswahili katika channel hii. Subscribe sasa na bofya alama ya kengere inayotokea baada ya Subscribe. Fungua Link hii .