• 7 years ago
Gospel Music Swahili | "Njia Yote Pamoja na Wewe" Mungu ni Upendo

Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini.
Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza.
Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako,
nina amani kabisa.
Unanibariki, Unatoa maneno Yako ya hukumu.
Bado sijui jinsi ninavyokosa kuithamini neema Yako.
Kila mara nikiasi, kwa namna fulani nikiuumiza moyo Wako.
Na bado Hunitendei kulingana na dhambi
zangu lakini Unafanya kazi kwa ajili ya wokovu wangu.
Ninapokuwa mbali, Unaniita nirudi kutoka hatarini.
Ninapoasi, Unauficha uso Wako, giza likinifunika.
Ninaporudi Kwako,
Unaonyesha neema, Unatabasamu ili kukumbatia.
Shetani anaponipiga,
Unatibu vidonda vyangu, Unaupa joto moyo wangu.
Shetani anaponiumiza,
Uko nami kuanzia mwanzo hadi mwisho wa majaribu.
Alfajiri itafika karibuni,
na anga itang’aa samawati kama awali,
wakati Uko nami.
Alfajiri itafika karibuni,
anga itang’aa samawati kama awali,
wakati Uko nami.

Wewe ni uhai wangu, Wewe ni Bwana wangu.
Mwenzi wa kila siku, kivuli cha karibu kando yangu.
Ukinifunza jinsi ya kuwa binadamu
na kunipa ukweli na uhai.
Pamoja na Wewe maisha yangu yanasonga mbele kwa utukufu . ...

kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Uimbe Nyimbo Mpya

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Barua Pepe: contact.sw@kingdomsalvation.org
Wasiliana Nasi: +254-700-427-192

Category

🎵
Music

Recommended